Saturday, August 11, 2018

UJASIRIAMALI 4

MAMBO YANAYOZINGATIWA KATIKA KUCHAGUA MUUNDO WA BIASHARA NI PAMOJA NA:

·         Masharti ya kisheria

·         Uwajibikaji wa wamiliki kwa madeni ya biashara

·         Aina ya shughuli za biashara

·         Mgawanyo wa mapato

·         Mahitaji ya mtaji

·         Idadi ya wafanyakazi na utawala

·         Manufaa na hasara za kihasibu/ kikodi

·         Urefu wa mzunguko wa biashara


UJASIRIAMALI 3

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA NDOGO
Biashara yoyote huanza na wazo, ila wazo pekee halitoshi, linahitaji kufanyiwa kazi. Hapo ndipo watu wengi huweza kuanza kujisikia kuzidiwa. Si ajabu kuona mtu anakatishwa tamaa kwa kutizama msururu wa mambo yanayohitajika ili kuanzisha biashara, lakini pia kuanzisha biashara ni rahisi kuliko unavyodhani. Kama ilivyo katika lengo lolote kubwa, ukianza kwa kutengeneza malengo madogo madogo ya kutekeleza utaweza kufanya mambo yote muhimu katika kuanzisha biashara.

Kuanzisha na kuendesha biashara inahitaji msukumo, nia na kipaji. Inahitaji pia utafiti na mipango. Kama ilivyo kwenye mchezo wa drafti, mafanikio kwenye biashara ndogo huanza na maamuzi sahihi katika hatua za mwanzoni. Ikumbukwe pia hapa kuwa pamoja na kwamba makosa madogomadogo ya mwanzoni yanaweza yasiue biashara yako, inahitaji ujuzi, nidhamu, na bidii kuyasahihisha.
Ili kuboresha uwezekano wa kufanikiwa, unapaswa kutenga muda wa kujichunguza na kutathmini malengo yako kibiashara na malengo binafsi. Tumia taarifa hiyo kutengeneza kwa umakini mkubwa mpango wa biashara ambao utakuwezesha kufikia malengo yako.
Mchakato wa kuandaa mchanganuo wa biashara utakuchochea kufikiria hata baadhi ya mambo ambayo usingekumbuka kuyafikiria katika hali ya kawaida. Mchanganuo wako utakuwa zana muhimu sana unapopambana kutafuta fedha kwa ajili ya biashara yako. Mchanganuo huo pia unaweza kutumika kama kigezo cha kila mara kufuatilia/ kupima mafanikio ya biashara yako.
Yako mambo kadhaa yanayohitajika katika biashara yoyote.

Jambo la kwanza kabla ya kuanzisha biashara ni kuwa unatakiwa ujiulize sababu za wewe kutaka kuingia kwenye biashara. Sababu zilizozoeleka za kuanza biashara ni:
·         Unataka kujiongoza mwenyewe.
·         Unataka uhuru wa kifedha.
·         Unataka uhuru wa kutumia ubunifu wako.
·         Unataka kutumia kikamilifu ujuzi na ufahamu wako

Jambo la pili ni kuamua biashara ipi inakufaa? Ili kufahamu ni biashara ipi inakufaa, jiulize maswali yafuatayo:
·         Ninapenda kutumiaje muda wangu?
·         Nimejifunza au kusomea ujuzi gani?
·         Watu wengine wanazungumzia ubora wangu kwenye mambo gani?
·         Nina muda kiasi gani kuendesha biashara kwa ufanisi?
·         Katika mambo ninayopendelea yapo ambayo yanaweza yakawa fursa ya biashara?
·         Biashara yangu itahudumia sehemu/ kundi gani katika soko?
·         Je? Wazo langu linatekelezeka na litakidhi hitaji katika soko?
·         Ushindani nilionao ni upi? Nami nina uwezo gani katika ushindani?
·         Biashara yangu ina manufaa gani kuzidi zingine zilizopo?
·         Je? Naweza kutoa huduma zenye ubora zaidi?
·         Je? Naweza kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa/ huduma zangu?

Ukishapata majibu ya maswali hayo hapo juu ni wazi kuwa utakuwa ulishaanza kujua ni biashara gani unaweza kuianzisha. Lakini pia unatakiwa ujiulize maswali haya hapa ili kuwa na uhakika na biashara ambayo utaifanya.
·         Ninakusudia kuanzisha Biashara gani?

·         Nitauza bidhaa gani au nitatoa huduma gani?

·          Biashara nitafanyia eneo gani?

·         Nitatumia ujuzi na uzoefu gani kwenye biashara?

·         Biashara yangu itakuwa na muundo gani kisheria?

·         Niiite biashara yangu jina gani?

·         Nitatumua vifaa gani, na nitakuwa na mahitaji gani?

·         Nahitaji bima ya aina gani?

·         Nahitaji fedha kiasi gani?

·         Nina rasilimali zipi?

·         Nitajilipaje?

Majibu yako yatasaidia kutengeneza mpango makini, uliofanyiwa utafiti wa kutosha, ambao utautumia kama ramani ya kuelekeza kila hatua katika utekelezaji wa biashara na hata kupata mtaji.
Chagua muundo sahihi wa biashara yako.
Unapoanzisha biashara yoyote, mojawapo ya maamuzi muhimu sana ya kufanya ni uchaguzi wa muundo wa hiyo biashara.


UJASIRIAMALI 2

KABLA YA KUANZISHA BIASHARA YAKO HAKIKISHA UNA SIFA ZIFUATAZO:
Nidhamu binafsi – Hakuna mjasiriamali anayependa kuona biashara yake inakufa, kila mmoja analenga kuhakikisha biashara inafanikiwa na huondosha kila jambo linaloweza kuhatarisha ustawi wa biashara husika. Wajasiriamali waliofanikiwa wana nidhamu ya kuchukua hatua kila siku kuelekea kwenye kufanikisha malengo yao. Hakikisha unanidhamu ya kutunza mda na nidhamu ya kutumia pesa zinazopatikana kutokana na biashara yako.
Kujiamini – Mjasiriamali hupaswi kuwa na wasiwasi kuwa unaweza kufanikiwa au la, unapaswa kujiamini mda wote kuwa utafanikisha biashara yako. Jitahidi kudhihirisha kujiamini huko kwa kufanya kazi kwa bidii ili kifikia malengo uliyojiwekea.

Muwazi wa fikra – Mjasiriamali anatambua kuwa kila tukio au hali ni fursa ya kibiashara. Mawazo mapya yanaibuliwa kila mara kuhusu mtiririko wa kazi na ufanisi, ujuzi, na biashara mpya. Mjasiriamali ana uwezo wa kutizama kila jambo [hali/ tukio] linalomzunguka na kulitumia kufanikisha lengo lake.

Muanzilishi  Mjasiriamali anafahamu kuwa kama kuna jambo linalopaswa kufanyika basi yeye mwenyewe ndiye anayepaswa kulianzisha. Hujiwekea vigezo na kuhakikisha biashara inafuata kuelekea kutekeleza/ kukidhi vigezo hivyo. Wako makini katika kutwaa fursa bila kuhitaji kusubiri mtu mwingine awape fursa

Mshindani – Chanzo cha biashara nyingi ni mjasiriamali mmoja kutambua kuwa anaweza kufanya biashara hiyo kwa ubora kuliko mwingine/ wengine. Wajasiriamali wanahitaji kufanikiwa katika biashara wanazoanzisha mithili ya mchezaji anavyohitaji kushinda katika mchezo anaocheza. Mjasiriamali ni mwepesi kuonesha namna taasisi yake ilivyofanikiwa katika hatua mbalimbali.

Mbunifu – mojawapo ya mambo muhimu katika ubunifu ni kumudu kuunganisha mambo ambayo hayaonekani kuwa na uhusiano katika kutengeneza fursa. Wajasiriamali huja na suluhisho baada ya kuchambua na kutengeneza uhusiano wa hali/ matukio mbalimbali. Huweza hata kubadili malengo ya bidhaa fulani na kuiuza katika soko tofauti.

Kutokata tamaa – Wajasiriamali hawakatishwi tamaa na kushindwa. Kila anaposhidwa huichukulia kama fursa ya kujifunza na kufanikiwa. Wanatamani kila wanalofanya lifanikiwe, hivyo hujaribu tena na tena hadi wafanikiwe. Hawaamini kuwa kuna jambo lisilowezekana

Ujuzi binafsi – Mjasiriamali ana ujuzi mzuri wa kuwasiliana katika kuuza na kuwapa motisha waajiriwa wao. Wajasiriamali wengi waliofanikiwa hufahamu namna ya kuwapa motisha waajiriwa wao hivyo kukuza biashara zao. Ni wazuri katika kuelezea faida za hali mbalimbali na kuwafundisha wengine katika kufanikiwa.

Mwenye kuheshimu maadili ya kazi yake – Mjasiriamali hufanikiwa kwa kufuata/ kutii kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Mifano ya wajasiriamali wasio na maadili ni: Muuzaji wa matunda anayeokota matunda kutoka kwenye shimo la taka kwa ajili ya kuwatengenezea wateja wake sharubati (juisi), au mjasiriamali anayeuza nyama isiyokaguliwa au iliyokatazwa kwa matumizi ya binadamu.

Mwenye kupenda kazi yake – Kupenda na kuthamini kazi yake ni sifa muhimu kuliko zote anayohitaji mjasiriamali ili kufanikiwa. Mjasiriamali ana mapenzi ya dhati kwa kazi yake. Yuko tayari kufanya kazi saa za ziada kuhakikisha biashara yake inafanikiwa, maana hupata furaha kuona biashara inafanikiwa. Mjasiriamali anayefanikiwa ni yule ambaye hujifunza bila kuchoka na kutafiti namna mbalimbali za kufanya biashara yake iwe bora zaidi.

Wajasiriamali wanaofanikiwa hutizama biashara zao kama mtu aliye juu ya kilima na kuona biashara yake ilivyo. Akishaiona, anataka kwenda mbali zaidi. Wanafahamu namna ya kuzungumza na waajiriwa wao, na biashara zao hutanuka kwa sababu hiyo.

UJASIRIAMALI 1

MWONGOZO WA KUANZISHA BIASHARA
http://entrepreneurs.or.tz/wp-content/uploads/2015/11/kuku1-300x188.jpg
Baada ya kupata cheti cha namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.
Uchumi wa Tanzania umekuwa ukizalisha ajira chache kila siku. Hii imekuwa ikifanya vijana wengi wanaohitimu vyuoni kubaki wakizunguka na bahasha kila kona kusaka ajira.
Takwimu kutoka ofisi ya takwimu ya taifa zinaonyesha kuwa mwaka 2014 taifa lilizalisha nafasi za ajira 282,382 tu ukilinganisha na mahitaji ya zaidi ya wahitimu 400,000 wanaomaliza vyuo kila mwaka.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa Tanzania kama nchi inahitaji kuweka nguvu za ziada katika kuhakikisha kuwa nafasi zaidi za ajira zinatengenezwa.
Pengine njia pekee inayoweza kutumiwa kupunguza tatizo hili au hata kulimaliza kabisa ni kupitia ajira binafsi (Ujasiriamali).
Pamoja na kuwa ujasiriamali unaweza kuwa suluhisho la ajira nchini, vijana wengi wameshindwa kabisa kufanya ujasiriamali kutokana na kukosa elimu sahihi. Kwa bahati mbaya sana mfumo wetu wa elimu haumsaidii sana muhitimu kupata stadi za ujasiriamali.
Katika vipaumbele vyake, Rais John Magufuli anasisitiza sana Tanzania ya viwanda, lakini hili litatokea tu kama vijana wa kitanzania watapatiwa elimu ya ujasiriamali.

Sehemu hii itakuwa ikiwapatia makala mbalimbali za ujasiriamali… tutajifunza jinsi ya kuanzisha biashara, jinsi ya kuendeleza biashara yako na namna ya kupata fedha.

Thursday, August 2, 2018

REVISION QUESTIONS

FORM FOUR GOLDEN GROUP (HEROES)
ENGLISH LANGUAGE
TASK NUMBER THREE (3) FRIDAY 27/04/2018
QUESTIONS:
1.    Africa is one in terms of environment and experience. Take two readings you have done under this section and verify the above statement.

2.    “It is right time for us to look back into our cultural aspects for the purpose of modifying them.” Do we need to modify our culture? Use two plays support your answer.

3.    Many novel writers usually use their pens to show different problems existing in the society. Use two novels to show different social problems portrayed by the authors.

4.    Authors usually choose book titles which cover much information of what is contained in their books. Choose two titles of the books you have read and explain their relevance to the stories in those books.

5.    Diction refers to the choice and use of language in a literary work. Use two novels to show the language techniques used.



PUSH for your better future.

PUSH means (Pray Until Something Happens).