MWONGOZO
WA KUANZISHA BIASHARA
Baada ya kupata cheti cha
namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara
kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na
Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.
Uchumi wa Tanzania umekuwa
ukizalisha ajira chache kila siku. Hii imekuwa ikifanya vijana wengi
wanaohitimu vyuoni kubaki wakizunguka na bahasha kila kona kusaka ajira.
Takwimu kutoka ofisi ya takwimu
ya taifa zinaonyesha kuwa mwaka 2014 taifa lilizalisha nafasi za ajira 282,382
tu ukilinganisha na mahitaji ya zaidi ya wahitimu 400,000 wanaomaliza vyuo kila
mwaka.
Hii
inaonyesha dhahiri kuwa Tanzania kama nchi inahitaji kuweka nguvu za ziada
katika kuhakikisha kuwa nafasi zaidi za ajira zinatengenezwa.
Pengine
njia pekee inayoweza kutumiwa kupunguza tatizo hili au hata kulimaliza kabisa ni
kupitia ajira binafsi (Ujasiriamali).
Pamoja
na kuwa ujasiriamali unaweza kuwa suluhisho la ajira nchini, vijana wengi
wameshindwa kabisa kufanya ujasiriamali kutokana na kukosa elimu sahihi. Kwa
bahati mbaya sana mfumo wetu wa elimu haumsaidii sana muhitimu kupata stadi za
ujasiriamali.
Katika
vipaumbele vyake, Rais John Magufuli anasisitiza sana Tanzania ya viwanda,
lakini hili litatokea tu kama vijana wa kitanzania watapatiwa elimu ya
ujasiriamali.
Sehemu hii itakuwa ikiwapatia makala
mbalimbali za ujasiriamali… tutajifunza jinsi ya kuanzisha biashara, jinsi ya
kuendeleza biashara yako na namna ya kupata fedha.
No comments:
Post a Comment