JINSI YA KUANZISHA BIASHARA NDOGO
Biashara
yoyote huanza na wazo, ila wazo pekee halitoshi, linahitaji kufanyiwa kazi.
Hapo ndipo watu wengi huweza kuanza kujisikia kuzidiwa. Si ajabu kuona mtu
anakatishwa tamaa kwa kutizama msururu wa mambo yanayohitajika ili kuanzisha
biashara, lakini pia kuanzisha biashara ni rahisi kuliko unavyodhani. Kama
ilivyo katika lengo lolote kubwa, ukianza kwa kutengeneza malengo madogo madogo
ya kutekeleza utaweza kufanya mambo yote muhimu katika kuanzisha biashara.
Kuanzisha
na kuendesha biashara inahitaji msukumo, nia na kipaji. Inahitaji pia utafiti
na mipango. Kama ilivyo kwenye mchezo wa drafti, mafanikio kwenye biashara
ndogo huanza na maamuzi sahihi katika hatua za mwanzoni. Ikumbukwe pia hapa
kuwa pamoja na kwamba makosa madogomadogo ya mwanzoni yanaweza yasiue biashara
yako, inahitaji ujuzi, nidhamu, na bidii kuyasahihisha.
Ili
kuboresha uwezekano wa kufanikiwa, unapaswa kutenga muda wa kujichunguza na
kutathmini malengo yako kibiashara na malengo binafsi. Tumia taarifa hiyo
kutengeneza kwa umakini mkubwa mpango wa biashara ambao utakuwezesha kufikia
malengo yako.
Mchakato
wa kuandaa mchanganuo wa biashara utakuchochea kufikiria hata baadhi ya mambo
ambayo usingekumbuka kuyafikiria katika hali ya kawaida. Mchanganuo wako
utakuwa zana muhimu sana unapopambana kutafuta fedha kwa ajili ya biashara
yako. Mchanganuo huo pia unaweza kutumika kama kigezo cha kila mara kufuatilia/
kupima mafanikio ya biashara yako.
Yako
mambo kadhaa yanayohitajika katika biashara yoyote.
Jambo la kwanza
kabla ya kuanzisha biashara ni kuwa unatakiwa ujiulize sababu za wewe kutaka
kuingia kwenye biashara. Sababu zilizozoeleka za kuanza biashara ni:
·
Unataka kujiongoza mwenyewe.
·
Unataka uhuru wa kifedha.
·
Unataka uhuru wa kutumia
ubunifu wako.
·
Unataka kutumia kikamilifu
ujuzi na ufahamu wako
Jambo la pili
ni kuamua biashara ipi inakufaa? Ili kufahamu ni biashara ipi inakufaa, jiulize
maswali yafuatayo:
·
Ninapenda kutumiaje muda wangu?
·
Nimejifunza au kusomea ujuzi
gani?
·
Watu wengine wanazungumzia
ubora wangu kwenye mambo gani?
·
Nina muda kiasi gani kuendesha
biashara kwa ufanisi?
·
Katika mambo ninayopendelea
yapo ambayo yanaweza yakawa fursa ya biashara?
·
Biashara yangu itahudumia
sehemu/ kundi gani katika soko?
·
Je? Wazo langu linatekelezeka
na litakidhi hitaji katika soko?
·
Ushindani nilionao ni upi? Nami
nina uwezo gani katika ushindani?
·
Biashara yangu ina manufaa gani
kuzidi zingine zilizopo?
·
Je? Naweza kutoa huduma zenye
ubora zaidi?
·
Je? Naweza kutafuta soko kwa
ajili ya bidhaa/ huduma zangu?
Ukishapata
majibu ya maswali hayo hapo juu ni wazi kuwa utakuwa ulishaanza kujua ni
biashara gani unaweza kuianzisha. Lakini pia unatakiwa ujiulize maswali haya
hapa ili kuwa na uhakika na biashara ambayo utaifanya.
·
Ninakusudia kuanzisha Biashara
gani?
·
Nitauza bidhaa gani au nitatoa
huduma gani?
·
Biashara nitafanyia eneo gani?
·
Nitatumia ujuzi na uzoefu gani
kwenye biashara?
·
Biashara yangu itakuwa na
muundo gani kisheria?
·
Niiite biashara yangu jina
gani?
·
Nitatumua vifaa gani, na
nitakuwa na mahitaji gani?
·
Nahitaji bima ya aina gani?
·
Nahitaji fedha kiasi gani?
·
Nina rasilimali zipi?
·
Nitajilipaje?
Majibu yako yatasaidia
kutengeneza mpango makini, uliofanyiwa utafiti wa kutosha, ambao utautumia kama
ramani ya kuelekeza kila hatua katika utekelezaji wa biashara na hata kupata
mtaji.
Chagua muundo sahihi wa
biashara yako.
Unapoanzisha biashara yoyote,
mojawapo ya maamuzi muhimu sana ya kufanya ni uchaguzi wa muundo wa hiyo
biashara.
No comments:
Post a Comment